Ugonjwa wa homa ya nguruwe umelipuka tena mkoani Mbeya na kuua zaidi ya nguruwe 900 katika wilaya za Mbeya na Rungwe.
Mganga
Mkuu wa Mifugo Mkoani Mbeya, Solomon Nong'ona akizungumza nasi jana
alisema, ugonjwa huo umerudi tena baada ya kuzuka kwa mara
ya kwanza Januari mwaka huu na kutokomezwa.
Alisema kufuatia kuzuka tena kwa ugonjwa huo, serikali kupitia sekta ya
mifugo imepeleka dawa mkoani humo ambazo zinasaidia kupunguza kasi ya
kuenea.
Nong'ona alisema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo wananchi nao
wanajitahidi kununua dawa hizo ili kuudhibiti na kuwakinga nguruwe
wanaowafuga.
Alisema ugonjwa wa homa ya nguruwe bado haijathibitika kuwa na madhara
kwa binadamu, hivyo wananchi wanaruhusiwa kula nyama ya nguruwe lakini
aliyechinjwa katika machinjio rasmi na kuthibitishwa na daktari wa
mifugo.
"Nguruwe hawa wanaweza kuliwa lakini wananchi wawe waangalifu kula nyama
hizo kwani kula myama ambaye amekufa mwenyewe ni hatari kwani huenda
amekufa kwa ugonjwa mwingine," alisema Nong'ona.
Alisema ugonjwa huo ulianza katika wilaya ya Mbeya na baadaye katika wilaya ya Rungwe.