KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka madiwani wa Mkoa wa Arusha kuhudhuria vikao vya madiwani walivyokuwa wamesusia kwa miaka kadhaa.
Imeeleza
kuwa kuanzia sasa waanze kuhudhuria vikao hivyo kutokana na wao kuwa
wengi na nguvu katika kupinga masuala kadhaa katika vikao hivyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema hayo jana wakati akitoa maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika juzi.
Alisema
baada ya kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu mkoani hapo kamati kuu
imeamua kuondoa pingamizi hilo la kutohudhuria vikao vya madiwani katika
Manispaa ya Arusha.
“Sasa
tumewaelekeza madiwani wote wa manispaa hiyo na wabunge kushiriki vikao
na kwa kutumia vikao hivyo kusimamia mali za umma na kupinga masuala
mbalimbali ndani ya baraza na siyo nje,” alisema.
Mbowe
alisema Kamati Kuu imeamua hivyo baada ya kuona madiwani wao wamekuwa
wengi kuliko vyama vyote vikiungana katika manispaa hiyo jambo
litakalosaidia katika kusimamia masuala yao.
Mbowe
alisema Kamati Kuu imewaagiza madiwani na wabunge kuzungumza na
wananchi wa manispaa hiyo na kuwaeleza bayana nia ya kuondoa pingamizi
hiyo.
“Wanatakiwa
kufanya hivyo haraka kwani wananchi wetu hawataki viongozi wao
kuhudhuria vikao hivyo ambavyo havina tija kwa maendeleo ya manispaa
yao,”alisema.
Alisema
sasa mapambano yamehamishiwa ndani ya baraza hilo na siyo nje ya ukumbi
kama ilivyokuwa hapo awali ili kukabiliana na ufisadi unaofanya katika
baraza hilo.
>>Habarileo
>>Habarileo
