Habari za kusikitisha kutoka wilayani makete mkoani Njombe zinaeleza kuwa , mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha maafa kwa kuezua mapaa ya nyumba zaidi ya 8 zilizopo katika kijiji cha Ndulamo wilayani hapo majira ya saa 10 jioni ya leo
Kwa mujibu wa ripota wa mtandao huu wa eddymoblaze.blogspot.com aliyefika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu na wananchi hao, amesema haijafahamika mara moja kama tatizo hilo limesababisha vifo ama madhara makubwa kiasi gani
Mwandishi huyo ameshuhudia mabaki ya vipande vya mabati yaliyokuwa yamekwama juu ya miti iliyopo jirani na eneo hilo
katika hali iliyoacha watu wengi midomo wazi, mapaa yaliyoezuliwa katika nyumba hizo hayajaonekana eneo la tukio licha ya kuonekana vipande vya mabati peke yake lakini si mbao
Kufuatia hali hiyo, mbunge wa Makete ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais - mazingira Dkt Binilith Mahenge amefika eneo la tukio na kujionea hali halisi huku akitoa kiasi cha shilingi 100,000/= taslimu kisaidie wahanga wa tukio hilo
Dkt Mahenge ambaye ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya wakiwemo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete wameonesha kuguswa na tatizo hilo huku nao wakitoa michango yao kwa wahanga wa tukio hilo
Amewaahidi kuwa serikali itatathmini tatizo hilo mara moja na pia kiasi cha fedha kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya maafa hayo kitatolewa kusaidia walioguswa na tatizo hilo
taarifa zidi utazidi kuzipata hapa hapa ikiwemo picha za tukio hilo, tunaomba uwe na subira mpendwa msomaji wetu