MENEJA wa hotel ya
Mediteranian iliyoko Kawe Beach jijini Dar es salaam aliyepigwa makofi
na kutukanwa na beautiful Onyinye wa bongo movies Wema Isack Sepetu
amesema kuwa ameshampata wakili mkubwa wa kumsaidia katika rufaa ya kesi
yake na kwamba sasa kesi hiyo itasimamiwa kwa ushirikiano na mabosi
wake.
Akiongea na Swahilitz meneja huyo ambaye hakuridhika na hukumu ya Wema kutoa laki moja na kumaliza kesi katika mahakama ya mwanza ya Kawe chini ya mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda.
Akiongea na Swahilitz meneja huyo ambaye hakuridhika na hukumu ya Wema kutoa laki moja na kumaliza kesi katika mahakama ya mwanza ya Kawe chini ya mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda.
"Unajua mara ya kwanza
niliambiwa siwezi kushindanan na Wema kutokana na mwanja mkubwa aliokuwa
nao lakini nilimuomba Mungu anisaidie kwa hilo kwasababu kwa Mungu
hakuhitaji hela, nimesimama kidete na kumuomba Mungu na sasa kesi
nairudisha upya kwani wakili niliyempata na wa kizito na ni wa uhakika"
alisema meneja huyo.
Alifafanua kuwa katika
rufaa yake atakuwa sambamba na wakili huyo pamoja na wamiliki wa hotel
ya Mediteranian ambao kwa pamoja wameahidi kuhakikisha suala hilo
linapatia ufumbuzi yakinifu.
Wema alipandishwa
kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda
na kudaiwa kufanya vurugu kushambulia na kumpiga makofi na kumtukana
bwana Goodluck Kayumbu.
Hata hivyo katika katika kujitetea alidai kuwa yote yalifanyika kwasababu ya pombe na sio kwa masudi
Hatua ya bwana Kayumbu
kukimbilia rufaa katika kesi ambayo ilishamalizika ni pigo la pili kwa
Wema ndani ya mwaka huu kwani hivi karibuni imeelezwa kuwa alikumbwa na
mkosi baada ya mahakama ya Ilala kuamuru anyang'anywe gari lake la
kifahari aina ya Audi Q7 lenye usajili wa T973 BUJ na kukabidhiwa kwa
mmiliki wa gari hilo.
