Wananchi katika
manispaa ya Iringa wametakiwa kuweka mazingira katika hali ya usafi kwa kipindi
hiki cha msimu wa mvua, ili kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Hayo yamesemwa na
Afisa afya wa manispaa ya Iringa, MERCY KINENEKEJU ,na kusema
kuwa wananchi wanatakiwa kufanya usafi nje ya makazi yao na kutupa taka sehemu
husika.
KINENEKEJU ameongeza kuwa
kutokana na changamoto waliyonayo ya magari ya kubebea taka, wanafanya jitihada
za kupata magari kupitia mradi wa Word Bank ifikapo FebruarI mwaka huu watapata
msaada wa gari moja ili kupunguza mlundikano wa taka katika baadhi ya maeneo.
Wakati huohuo
ameviomba vyombo vya habari kuzidi kutoa elimu kwa wananchi juu ya usafi wa
mazingira ili kuweka manispaa katika hali ya usafi.