Wananchi mkoani Iringa
wameombwa kuwachukia vibaka na kuwafichua kwa kushirikiana na jeshi la polisi
kulinda usalama wa mkoa kwa kuwadhibiti na kuwamaliza .
Hayo yamesemwa na
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, RAMADHAN MUNGI na kusema
kuwa vibaka hao wanafahamika na endapo wananchi watawafichua watasaidia
kuwadhibiti na kuwafanya wafanyabiashara na wananchi kuishi kwa usalama.
Kamanda amesema kuwa
jeshi la polisi linaupungufu wa polisi na maeneo mengi yanavibaka, hivyo
linahitaji msaada wa wananchi katika kutenda kazi kwani bila ushirikiano wao
hawataweza kuwadhibiti.
Hata hivyo amesema
kuwa kwa ushirikiano huo kutasaidia kuweka mikakati ya kuzuia uhalifu katika
mkoa ,kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutunza amani ya nchi yetu.
Aidha ameongeza kwa
kusema kuwa hali ya usalama katika mkoa wa Iringa ni nzuri kwa sasa na uhalifu
unazidi kupungua huku akisisitiza ushirikiano ili kulinda usalama.
