Stori: ISSA MNALLY NA DUSTAN SHEKIDELE
OPARESHENI ya Polisi wa Mkoa wa Morogoro na kikosi maalum cha kufichua
Maovu cha Magazeti ya Global Publishers (OFM), imemnasa mwanamke
mjamzito katika kamatakamata ya machangudoa.
Polisi akimkagua changudoa mwenye mimba aliyenaswa akijiuza.
Katika oparesheni hiyo ya aina yake iliyofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika eneo la Msamvu (Kambi ya Itigi), wanawake 30 waliodaiwa
kujihusisha na biashara hiyo walikamatwa.
Waandishi wetu wakiwa na askari wa mkoa huo walimnasa mjamzito huyo
anayedaiwa kuwa na mimba ya miezi sita akiwa mawindoni eneo hilo.
Changudoa huyo mwenye mimba akiwa chini ya ulinzi.
Mara baada ya mjazito huyo kukamatwa alitoa yake ya moyoni kwa kusema
kwamba anafanya biashara hiyo ili kupata fedha za kujikimu na ujauzito
wake haumpi shida yoyote.
“Jamani natafuta pesa za kujikimu na maisha hapa mjini sasa
mnatukamata tukale wapi? Hii mimba ni yangu na ninayefanya ukahaba ni
mimi niacheni,” alisema mdada huyo.
Pamoja na maneno yake, polisi walimbeba msobemsobe na kumfikisha kituoni pamoja na makahaba wengine.
CREDITS; GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi