Wananchi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kujijengea utaratibu wa
Kujisomea Vitabu Mbalimbali kwani ni
Njia Moja wapo yakuongeza Maarifa.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu mstafu wa Dayosisi ya kusini Kati Dkt
Solomon Swalo (pichani)katika Tafrija ya kumpongeza baada ya kutunukiwa shahada ya
Uzamivu (PHD) iliyofanyika Bulongwa Makete
Dk Swalo ambaye pia ni mwandishi mahili wa vitabu amesema amekuwa
akiandika vitabu mbalimbali kwaajili ya kuweka kumbukumbu ya vizazi vilivyopo
na vijavyo lakini hakuna wasomaji wa vitabu hivyo.
Akizungumza kwaniaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Makete mh. Josephine
Matiro Amesikitishwa natabia ya Baadhi ya watu na Tabia ya kuto kupenda kusoma
Vitabu na kuwataka wananchi kuanza kujisomea.
mh. Matiro amesema kuwa serikali ipo pamoja na kanisa ili kujiletea maendeleo
Hivyo anaimani mchango wa Askofu Mstaafu Dk Swalo Unahitajika sana katika Jamii.
Katika Hatua nyingine kanisa limempa Hati ya Jengo Askofu Dk Swalo
kwa ajili ya kuuzia Vitabu lililopo Eneo la Namanga Bulongwa.
Tukio Hilo la Kumpongeza Dk Swalo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa
Serikali, kanisa pamoja na wananchi.