Baadhi ya Wananchi wanaoishi katika manispaa ya Iringa wameiomba Serikali kukarabati
eneo la stendi ya Ipogoro kutokana na mazingira ya eneo hilo kutoridhisha, hususaN kipindi hiki cha mvua.
Wananchi
hao wameyasema hayo leo walipokuwa wakizungumza ana kwa ana na mshika
kalamu wa hapa jamvini,aliyefika eneo la tukio,na kujionea hali halisi
ya eneo hilo ambalo limeonekana kuwa kero kwa wakazi wake.
Baadhi ya Wananchi ambao ni Wafanyabiashara wa eneo hilo wamesema
kuwa mara kadhaa wamekuwa wakidaiwa ushuru kwa ajiri ya
kuboresha eneo hilo,lakini wanashangaa hakuna linalofanyika katika kuboresha stendi hiyo.
Aidha
wameitaka serikali kuboresha miundombinu ya eneo hilo la stendi ya
ipogoro ili kuraisisha utendaji kazi wa Wafanyabiashara hao na wakazi
wengine wa eneo hilo kwa ujumla sambamba na watumiaji wa kituo hicho
a.k.a abiria.
