Kufuatia kampeni za uchaguzi mdogo ambazo zitaanza kesho Chama cha
mapinduzi (CCM), kimesema kuwa kimejiandaa vizuri na kinauhakika wa kuchukua nafasi
hiyo.
Akizungumza na katibu wa CCM mkoa,Bwa Mtenga Husein amesema kuwa kura za maoni
kwa wagombea zimefanyika leo na wagombea wanakabidhi fomu hii leo
katika kata ya Nduli.
Katibu
amewataka wanachi kumchagua kiongozi atakayewaletea maendeleo na si
kufuata chama anachotoka,hii itapelekea kuwasaidia wananchi kumpata
kiongozi mwenye uadilifu, makini na mwenye kujituma katika suala zima
la kuleta na kujenga maendeleo kwa Wananchi wake halikadhalika kwa
maendeleo ya Taifa kiujumla.
Kwa
upande wa jeshi la polisi,akizungumza kamanda wa Mkoa wa Iringa
Ramadhani Mungi,amewaonya wanasiasa wote ambao watajinadi kuwania nafasi
hizo
kutumia lugha nzuri na zenye staha katika suala zima la kulinda amani na
utulivu kwa kipindi chote cha kampeni.Aidha ameongeza kwa kusema
kuwa kwa yoyote atakayetumia lungha itakayosababisha kuvunja amani
hawataweza
kumvumilia.
