Wenyeviti wa CCM mikoa ya Tanzania bara wametoa tamko la kumkana
Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti CCM Taifa Mgana Mzindakayi la kutowauza
wenyeviti wenzake kwa watu wanaotarajia kugombea urais kabla ya muda
na utaratibu wa Chama kufika.
Hatua hiyo inafuatia tamko lililotolewa kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM
wa mikoa ya Tanzania bara Joseph Msukuma leo jijini Mwanza kufuatia
kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msindayii ambaye ni mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Singida alipoalikwa kwenye sherehe ya kuuaga na kuukaribisha
mwaka mpya wilayani Monduli
Kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Mjumbe wa NEC na mbunge wa Monduli
Mhe. Edward Lowassa ambapo katika salamu zake Msindayi alinukuliwa na
vyombo vya habari na taarifa zake kutoka leo akisema kuwa yeye pamoja na
wenyeviti wa CCM wa mikoa yote nchini wako nyuma ya Lowassa wakimuunga
mkono kauli ambayo imewaweka katika wakati mgumu na wenyeviti wa CCM
mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kuanza kuwagawa na kutengeneza makundi.
hiki ndicho walichokisema wenyeviti Ccm Tanzania Bara 2014
