Hapa ndio hapapitiki kabisaaaaaa,ni bwawa la samaki.
Kwa mbali nafaka zikiwa zimetunzwa huku maji yakiwa yamezunguka eneo hilo.
Barabara ikiwa tope tupuuu hivyo kufanya ushushaji wa nafaka kuwa mgumu.
Hali ya barabara katika eneo la sido mkoani
Mbeya ni ya kutisha na kuhuzunisha sana. Eneo hilo ambalo limetengwa
maalumu na Jiji la mbeya kwa ajili ya stoo za wafanyabiashara na pia ni
maalumu kwa watu wanaohusika na ukoboaji, usagaji na kukamua mafuta ya
alizeti.
Ukifika eneo hilo kipindi cha kiangazi huwa ni kavu lakini kuna mashimo mengi yasiyorekebishwa.
Shida huwa inakuja kipindi cha masika na
mvua nyingi ambapo kupitika kwa maeneo yanayozunguka eneo hilo huwa ni
shida sana kwa waenda kwa miguu na pia magari makubwa na madogo
yanayoshusha na kupakia mizigo kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania.
Eneo hili pia ni kiungo muhimu sana kwa
wakazi wanaokaa maeneo ya uwanja wa ndege, kwa kuwa wengi wanatumia njia
hii kama ni shortcut ya kufika haraka majumbani mwao.
Dj sek blog ilifanya uchunguzi yakinifu kwa
takribani wiki moja eneo hili na kuweza kuvumbua mambo mengi sana,Moja
ya mambo hayo ni kwamba kwa kiasi kikubwa eneo hili hutumika kama makazi
yasiyo rasmi kwa watoto wa mitaani,ambao wengi hawana makazi au mahala
pa kulala.
Watoto hao wa mitaani hutumia majengo
ambayo hayajamalizika vizuri kujiihifadhi kama makazi yao,Mtandao wetu
ulifanya mahojiano na baadhi ya wamiliki wa mashine na stoo za eneo hilo
kubwa ni kutaka kujua kwa nini eneo hilo limetawaliwa na
madimbwi,mashimo makubwa na maji yaliyotuama kwa wingi.
Wafanyabiashara hao wameitupia lawama
uongozi wa jiji kwa kushindwa kusimamia vizuri eneo hilo ambalo
limetengwa maalumu kwa ajili yao, wakiongeza kuwa wanatoa kodi kila
mwaka,kila mwezi walitegemea kodi zao zitatumika kukarabati eneo hilo
lakini kinyume chake imekuwa ni shida kwao.
Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa magari
yanayokuja kushusha na kupakia yamekuwa yakipata sana shida kupita eneo
hilo hasa kipindi kama hiki cha mvua,hivyo wameiomba Serikali kuwasaidia
kukarabati eneo hilo.
Mtandao huuu ulijaribu kumtafuta mtu
anayeratibu na kusimamia eneo hilo lakini mpaka tunamaliza utafiti huu
hatukuweza kumpata.Rai ya mtandao wetu ni kwamba viongozi msikae tu huko
maofisini tokeni nje pia huku muone wanaicni wanavyokuwa na kero
nyingi.
(PICHA NA DJ SEK BLOG)



