HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia
zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi
kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji
huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari
13, mwaka huu.
Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa Mahakama kuu leo jioni.
Tundulisu akizungumza na waandishi nje ya mahakama
Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo
Wafuasi
wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakiwa wamekaa chini kutii amri ya
polisi baada ya matokeo ya kesi kutangazwa upende wao ukiwa aumeibuka
kidedea
Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wa chama hicho kutaka Zitto
atimuliwe uanachama, wakiwa wameduwaa nje ya mahakama baada ya uamuzi wa
Jaji, John
Mmoja wa wafuasi wa Chadema upande wa wanaounga mkono uongozi akiwa amejeruhiwa kichwani baada ya kupigwa jiwe.
Mbwa mkali wa polisi akiwa tayari kwa lolote.
Wafuasi wa Chadema wakivurumishana mawe Zitto alipowasili mahakamani
Wananchi wa kawaida wakilazimika kusalimisha maisha yao kwa kutimua mbio
baada ya wafuasi hao wa Chdema kuanza kuvurumishiana mawe Zitto
alipowasili Mahakama kuu.Picha zote na the nkoromo blog
Wafuasi
wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakiwa wamekaa chini kutii amri ya
polisi baada ya matokeo ya kesi kutangazwa upende wao ukiwa aumeibuka
kidedea








