| Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi |
Kikongwe mwenye umri kati ya
miaka 85 hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake amekutwa katika kijiji cha
Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kile
kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka usiku wakati akiwa kwenye
safari zake angani.
safari zake angani.
| Kikongwe huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi |
Kwa mujibu wa wakaazi wa
Kijiji hicho bibi huyo ameonekana leo majira ya saa 12 asubuhi akiwa katika
vichaka vilivyo kando ya barabara na alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa
anatoka Kijiji cha Nyihogo wilayani Kahama.
| Akiwa amelala chini kwa kile kinachodaiwa ni njaa |
Alipoendelea kuhojiwa alisema
alikuwa na wenzake na vitu mbalimbali ila wamemuacha, huku akisema hawezi
kuongea zaidi kwani anahisi njaa kwakuwa alikula toka jana tena chakula
Kibichi, jibu ambalo liliwashangaza wengi ni aina gani ya chakula ambacho
huliwa kikiwa kibichi.
Bibi huyo amekutwa na nguo
moja ya Kimasai na nguo zingine chache za kawaida lakini hakukutwa na vitu
vyovyote vinavyoashiria kuwa huenda ni mchawi, hivyo kuleta hisia kuwa huenda
alikuwa ni mtembea kwa miguu tu aliyepotea njia kwani watu wote wa eneo hilo
hakuna anayemtambua.
chanzo:dunia kiganjani