Msemaji wa Weusi, Nikki wa Pili
amekanusha kuachia wimbo unaoitwa ‘Ngalelo’ ambao umeonekana kwenye
baadhi ya blogs kama wimbo mpya wa rapper huyo.
“Kuna wimbo nimeona wametoa toa kwenye
mablog wameandika kwamba nimetoa wimbo wangu mpya, of course huo sio
wimbo. Kuna studio nilikuwa nimeenda nikafanya freestyle tu inaonekana
hao jamaa wameivujisha.” Nikki wa Pili ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Ni ile ile (studio) ya Afro Centric
lakini ni producer mwingine na sio producer ambaye yuko sasa hivi. Ni
kule maeneo ya Hostel karibu na chuo kwa hiyo nilikuwa na shindashinda
hapo.” Ameeleza Mweusi.
Hata hivyo, mkali huyo wa ‘Good Boy’ amesema kuna baadhi ya mistari katika hiyo freestyle iko katika nyimbo zake.
“Kuna baadhi ya mistari iko katika ngoma
zangu nyingine, lakini kwa kuwa wamelikisha mi naona sio issu, mimi
mashairi kwangu sio issue.”
Jana (January 3),Nikki wa Pili aliiambia tovuti ya Times Fm kuwa yeye na Joh wataachia wimbo wao wa pamoja February.
Source: http://timesfm.co.tz