Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa mh. Daniel Okoka ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo zikiwemo, maji, umeme, barabara, elimu, pamoja na matangazo ya redio
Kero hizo zimetolewe usiku wa kuamkia leo katika kipindi maalum cha Twanga swali Kitulo FM kinachorushwa na redio kitulo fm chini ya udhamini wa gazeti la daraja jana saa 1:15 hadi saa 3:20 usiku
Akijibu swali kuhusu elimu mh Okoka amesema wananchi wengi wamekuwa na mwamko mdogo kuhusu elimu kwani miongoni mwa wazazi wamekuwa wakishiriki kuwapeleka watoto mijini kufanya kazi mbalimbali badala ya kuwapeleka shule
Kuhusu miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami kutoka Njombe - makete amesema jitihada kubwa zimeshafanyika na kwa sasa upembuzi yakinifu umeshafanywa makete mjini na mara baada ya kumalizika kipindi hiki cha mvua za masika ujenzi utaanza mapema
Kwa upande wa umeme hasa kwa kata ya Tandala Okoka amesema nguzo tayari zimeshasimikwa, nyaya na transfoma nazo yatari zimewekwa hivyo kwa sasa kilichobakia ni kuunganisha kwenye gridi ya taifa kutoka Mbeya - makete na sasa zoezi hilo lipo ukingoni hivyo wananchi wawe na subira kidogo kwa kuwa linawezekana
Na Veronica Mtauka, Makete