JOHARI APOMBEKA KAMA 'KOMBA' KUFURAHIA RAY KUPIGWA CHINI...!SOMA ZAIDI HAPA...

Blandina Chagula ‘Johari’.
STAA wa kitambo kwenye filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amenaswa akipiga mitungi kwa sana ikiwa ni sehemu ya kufurahia uongozi mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity.

Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar ambapo uchaguzi wa safu mpya ya uongozi wa klabu hiyo ulimalizika na matokeo kuwatangaza mwenyekiti mpya Steven Mengele ‘Nyerere’ na wenzake kuwa washindi. 

Katika mahojiano na mwandishi wetu, Johari alisema: “Kwa upande wangu ninawaamini viongozi wote waliochaguliwa katika kutuletea maendeleo katika klabu yetu kwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano. Wote nawaamini na kusema kweli, hawa ndiyo viongozi tuliokuwa tunawataka
Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Katibu Mkuu Willium Mtitu, Katibu Msaidizi Devotha Mbaga, Mweka Hazina Issa Mussa ‘Cloud’ na msaidizi wake Sabrina Rupia ‘Cathy’.
 
-GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo