MLINZI AUAWA KIKATILI MKOANI NJOMBE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXcQY6AJslTCbL6Z9OyjFm-6SDqs-s769c8gTL9GRTsBEO5vU8N17Ufxd6sl0JpK-6i1R7H5HeK1vGd8tQKCekeQY4PDdWxWAnuZ0A9lpYXZ-lyzJKzyugFOa1NEh5zBim6a3s271S_DwM/s1600/RPC+NJOMBE.JPG
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani

 Mkazi wa Ulembwe Wilayani Wanging'ombe Steven Kiswaga Ameuwawa Kikatili  Kwa Kupigwa na Vitu Vizito Sehemu Mbalimbali za Mwili Wake Pamoja na Kukatwa Sikio la Upande wa Kulia na Watu Wasiofahamika .

Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Eneo la Tukio Wakazi wa Mtaa wa Ramadhan Wamesema Tukio Hilo Limetokea Usiku wa Kuamkia Leo Majira ya Saa Tisa Alfajiri na Kuongeza Kuwa Watu Hao Walifika Eneo la Duka Alilokuwa Akifanyakazi Marehemu Kama Mlinzi na Kisha Kufanya Unyama Huo na Kuutupa Mwili Wake Takribani Mita  100 Kutoka Eneo la Tukio, na Hapa Wanaeleza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kusema Kuwa Marehemu Alikuwa Akifanya Kazi ya Ulinzi wa Duka la Fred Mbilinyi Mkazi wa Mtaa wa Ramadhan, Kama Anavyoeleza Kamanda Ngonyani.

Hata Hivyo SACP Ngonyani Amesema Hadi Hivi Sasa Hakuna Mtu Ama Watu Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kuhusiana na Tukio Hilo na Kwamba Wanaendelea na Uchunguzi Ili Kuwabaini Watu Waliohusika na Tukio Hilo, Huku Mwenyekiti wa Mtaa wa Ramadhan Bashiry Sanga Akiwaomba Wananchi Kushirikiana Kukomesha Matukio ya Uhalifu. 


Na Gabriel Kilamlya


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo