skip to main |
skip to sidebar
LINAH NA SKENDO YA KUTEMBEA NA KIGOGO HADI KUMPA UJAUZITO
Na Musa Mateja
STAA wa Bongo Fleva, Estelinah
Sanga ‘Linah’ amepangua skendo inayomtafuna ya kutoka na kigogo mmoja wa
wizara nyeti ya Serikali ya Tanzania na kupachikwa ujauzito.
Estelinah Sanga ‘Linah’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Januari 17, mwaka huu, Linah alisema
shutuma hizo zimemwandama wakati siyo za kweli na hana uhusiano wa
kimapenzi na kigogo yeyote wa serikalini.
“Watu wamenizushia mambo kibao kuhusiana na ujauzito wakati sina na
wala sijawahi kuwa kwenye uhusiano na kigogo yeyote wa serikalini, hata
mtu anayetajwa sijawahi kumuona zaidi ya kumsikia tu.
“Naomba nieleweke kuwa nina mchumba wangu na anajulikana hadi kwetu,” alisema Linah.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi