HOT NEWS: POLISI WAUA KWA RISASI TARIME MKOANI MARA

Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya limefanikiwa kumuua jambazi sugu baada ya jambazi huyo kupambana na askari wa jeshi hilo kwa kurushiana risasi katika kitongoji cha Ntarechagini kijiji cha Nyamwaga Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Kamanda wa polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya Kamishina msaidizi Justus Kamgisha amesema baada ya jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa raia mwema na kuanza kumfuatilia jambazi huyo ndipo risasi zilianza kurushwa kutoka kichakani na kisha Polisi hao kujibu na kufanikiwa kumpiga Jambazi huyo.

Kamanda Kamgisha amemtaja jambazi huyo kuwa ni Senso Magabe Mwita ambaye alikuwa akitafutwa na Jeshi hilo kwa Makosa mbalimbali likiwemo la Mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo tukio la Mauaji lililotokea Desemba 30 na alikuwa na tabia ya kuleta majambazi toka nchi jirani ya Kenya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo