AKAMATWA AKIUZA DAWA ZA BINADAMU BILA KIBALI CHA TFDA

Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida imekamata madawa mbali mbali ya binadamu yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano yaliyokuwa yakiuzwa katika Kijiji cha Iglansoni na mtu asiyekuwa na sifa wala utaalamu huku duka hilo likiwa limefunguliwa kinyume cha utaratibu wa sheria za Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA).

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Bwana Magayane Protace amebainisha hayo wakati wa zoezi la kushitukiza lililofanyika katika Kata ya Iglansoni, tarafa ya Ihanja, kwa lengo la kubaini wafanyabiashara wa maeneo ya pembezoni wasiokuwa na leseni, wauzaji wa maduka ya madawa yasiyosajiliwa pamoja na Maabara bubu zilizofunguliwa kinyume cha sheria ya TFDA kwa lengo la kuwaibia wananchi.

AIDHA Bwana Magayane amesema muuzaji wa duka hilo Pendo Henry licha ya kutoa huduma za kuchoma sindano, hakuwa na cheti chochote na wala hajawahi kupata mafunzo ya awali ya kutoa huduma hizo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo