DK. SLAA : WANANCHI FANYENI UAMUZI MGUMU 2015

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema ili nchi iondokane na hali ya umaskini, wananchi wanatakiwa kufanya uamuzi mgumu wa kutoirudisha CCM madarakani, katika uchaguzi mkuu ujao, utakaofanyika mwakani.
Dk. Slaa alisema misingi mibovu ya CCM ndiyo sababu ya nchi kuyumba na kwamba hali hiyo imechangia Tanzania kuwa ya pili kutoka mwisho kwa umaskini barani Afrika, wakati nchi ipo katika nafasi ya pili kwa kuwa na rasilimali nyingi.

Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Siasa, katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni M4C Pamoja Daima.

Alisema, endapo wananchi watakubali kuwa na uamuzi mgumu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ikifika 2015 kwa kuipa Chadema nafasi ya kuongoza nchi, basi watambue kuwa wameondokana na hali hiyo ya umaskini.

“Kitu cha kwanza kukifanya pindi tutakapoingia Ikulu 2015 ni kuuza ndege ya Rais pamoja na mashangingi ya wabunge, ili fedha itakayopatikana tuipeleke kwenye shughuli za maendeleo,” alisema.

Dk. Slaa aliwapongeza wananchi kwa kutoa maoni yao ambapo wananchi milioni 3 na laki 3 walitoa maoni yao, huku asilimia 72 wakitaka ardhi ya Tanzania wamiliki wenyewe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo