MBUNGE WA IRINGA MJINI, MCH.MSIGWA AKANA TUHUMA ZA KUTOKABIDHI FEDHA ZA RAMBI RAMBI ZA DAUDI MWANGOSI

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha CHADEMA,Mch. PETER MSIGWA, amekanusha kuhusiana na tuhuma zinazomkabili juu ya kutokabidhi fedha za rambirambi kiasi cha shilingi milioni moja kwa mjane wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa marehemu DAUDI MWANGOSI, ambazo zilitolewa na wanachama wa CHADEMA waliopo nchini Uingereza na kusema kuwa tuhuma hizo si za ukweli, ni mambo ya uzushi na kwamba watu wanasema hivyo ili kumchafua.

Akizungumza na na kituo cha redio ya Nuru fm ya Iringa, kupitia kipindi cha sunrise power, Mh. MSIGWA amesema kuwa ni kweli pesa hizo alipokea kupitia kwa MAJID MGENGWA na baada ya kupokea fedha hizo alichangisha tena fedha kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini kupitia mkutano, ambapo walichangia kiasi cha laki tatu  pamoja na yeye mwenyewe aliongezea kiasi cha shiringi laki tano ,hivyo kupelekea kufikia kiasi cha shiringi milioni moja na laki nane na sitini na nane na kumkabidhi mjane wa marehemu  DAUDI MWANGOSI.

Msigwa amesema kuwa ni wanasiasa tu wanaojaribu kuwachafua baada ya kuona kuwa wameshindwa na tayari amewasiliana na uongozi wa chama chake ili kuweza kulichukulia hatua gazeti ambalo limeandika tuhuma hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo