KINANA NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA WASICHANA UKWAMA, MAKETE

Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana(kulia) akisalimiana na Bw. Titho Tweve ambaye analeta saruji ya kuendelea na ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya wasichana Ukwama, wa kwanza kushoto ni katibu NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye akifuatiwa na katibu wa NEC siasa na mahusiano ya kimataifa Dkt. Asharose Migiro
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (katikati) akitoa maelezo kwa katibu mkuu wa CCM kuhusu ujenzi wa shule hiyo
 Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kupata taarifa ya ujenzi huo, ambapo ameahidi kuwa chama cha mapinduzi kitatoa mabati 200 kwa ajili ya shule hiyo
Moja ya darasa la shule hiyo likiwa limekamilika kwa ujenzi
Msafara wa katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ukiondoka kwenye shule ya sekondari ya wasichana Ukwama, tayari kuelekea wilaya ya Wanging'ombe kwa ajili ya shughuli nyingine za kichama 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo