Leo huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwake na huku
akiomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri barani Afrika ndugu
Nelson mandela aliyetutoka hapo jana, mwanadada Jacqueline wolper
amenusufika kuumia kutokana na kupata ajali alipokuwa akisogeza gari
lake atoke kwenda kwenye mizunguko yake.
Jacqueline Wolper alipata ajali ya kugonga ukuta na kuharibu
gari lake alipokuwa akitaka kulitoa kwa kile alichosema kuwa ni makosa
ya kibinadamu kwani badala ya kukanyaga brake alijikuta akikanyaga pedal
ya mafuta kwa bahati mbaya kama alivyofunguka mwenyewe katika ujumbe
alioutoa hapo chini
“…dah kuzaliwa cku moja na kufa ni cku moja nando maana kila
cku nasisitiza upendo na chuki zisizokua na sababu.hvii leo ni bthday
yangu lakn nilikua nauvaa ukuta wakat nasogeza gar ioshwe tayar kwa
maandaliz .wakat nakanyaga brk kumbe nakanyaga mafuta maskn ya mungu
nimebomoa matnk ya maji yote nimepasua mabomba yote nimegonga gar
nyingne but yote nikumshukuru mungu kwakua sijaumia ila prsh ilishuka
kidogo but now npo ok.asante mwenyezi mungu,mungu wa wote,kimbilio la
wote na wewe ndo kimbilio langu.niombeeni maskn…”
Pole sana dada Wolper na Happy birthday kwako.
