Gari
aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt
Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na
utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa
kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa
wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani
Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki
shughuli mbalimbali za kijamii.
Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.
Pichani
Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka
kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya
Kimataifa iliponasa kwenye tope.
Katibu
wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa
amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara
baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na
mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendelea.
Eneo linavyoonekana
Gari
ikiwa imekwishaondolewa kwenye eneo korofi tayari kwa kuendelea na
msafara kutoka Wilaya ya Makete kuelekea Wilaya mpya ya
Wanging'ombe,mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa
ameambatana na Katibu wa NEC,ItIkadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa
NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro amemaliza ziara
yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa
Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR WA JIACHIE BLOG






