Pia
IGP Mwema, amemvisha cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi Diwani
Athumani ambaye alikuwa ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi.
Kufuatia
tukio hilo, IGP Mwema, amewaapisha Makamishina wanane kulingana na
nyadhifa zao mpya, ambapo Kamishina wa Polisi (CP) Clodwig Mtweve
ameapishwa kuwa Kamishina wa Fedha na Logistics, Kamishina wa Polisi
(CP) Paulo Changonja ameapishwa kuwa Kamishina wa Operesheni na Mafunzo,
Kamishina wa Polisi (CP) Mussa Ally Mussa ameapishwa kuwa Kamishina wa
Polisi Jamii na Kamishina wa Polisi (CP) Hamdani Makame ameapishwa kuwa
Kamishina wa Polisi Zanzíbar.
Wengine
ni Kamishina wa Polisi (CP) Issaya Mngulu ameapishwa kuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishina wa Polisi (CP) Thobías
Andengenye ameapishwa kuwa Kamishina wa Utawala na Utumishi, Kamishina
wa Polisi (CP) Abdulrahmani Kaniki ameapishwa kuwa Kamishina wa
Uchunguzi wa Sayansi ya Makosa ya Jinai na Kamishina wa Polisi (CP)
Ernest Mangu ameapishwa kuwa Kamishina wa Intelijensia ya Makosa ya
Jinai.
Kufuatia
kupandishwa vyeo na kupata nyadhifa mpya kwa Maafisa hao, Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua na kuthamini mchango wa
Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Aidha,
IGP Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo na walioteuliwa
katika nyadhifa mpya na kusema kuwa, kupitia vyeo na nyadhifa hizo ni
lazima Jamii ya watanzania iendelee kuwa salama, vitendo vya uhalifu
visiwe kikwazo cha jamii kujiletea maendeleo na kuhakikisha kwamba
usalama unashuka hadi ngazi ya familia.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.