



Ukifika maeneo ya makumbusho nyuma ya Jengo la Tigo maarufu mtaa wa kwa bwela kwa wauza viatu maarufu kwa wakina dada,hali ya usafi katika mitaro ya eneo hili ni ya kutisha ingawa imezungukwa na maofisi makubwa kama kampuni za simu na mabenki mengi.Dj sek blog ilifanya utafiti makini na kujione hali ya mitaro hiyo ikiwa katika hali mbaya kiusafi,Kwanza mitaro hiyo imeziba hivyo kusababisha maji kutuama na kupelekea maji hayo kuvunda na kuwa rangi ya njano.
Kingine cha kushangaza zaidi ndani ya mitaro hiyo watu hutumia kama
sehemu ya kutupia uchafu kama mifuko ya rambo,makopo n,k.Jambo lingine
ambalo ni la hatari zaidi ni eneo la juu ya mitaro hiyo kuna mgahawa
ambao unauza chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Jambo la
kujiuliza je watoa huduma katika mgahawa huo hawaoni hali hiyo ya uchafu
ambao upo kwenye eneo lao?na je hawaoni kwamba ni hatari kwa afya za
binadamu wanaokula eneo hilo?Tulipojaribu kuwauliza walikuwa hawana
majibu ya kutoa.Tunaomba serikali ya mtaa wa makumbusho walione hili na
kulishughulikia na sio kukaa ofisini mpaka magonjwa yatokee ndipo tuanze
kuhangaika.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG