NYERERE ALAANI KITENDO WANAFUNZI KUCHAPWA VIBOKO NA POLISI HUKO MARA

Na Shommi Binda, Mara — 
 
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini Vicent Nyerere amekasilishwa na kitendo cha kudhulumiwa kwa wanafunzi na kisha jeshi la polisi kuwafukuza kwa kuwachapa viboko na kusabababisha kutaharuki na kutawanyika ovyo barabarani, wakati walipoviendea vyombo  hivyo vya dola na viongozi wakitafuta kusaidiwa kuhusu michango wanayotozwa.

Nyerere alisema aliona adha iliyowapata wanafunzi hao kupitia vyombo vya Habari na kukilaani kitendo hicho na kusema ingetumika njia nyingine, "Wale wanafunzi walikuwa wanatafuta haki yao na hawakuwa na muongozo wowote wa walimu wala viongozi wa kuwasimamia.
 
 Haikupaswa kutandikwa viboko kama polisi walivyofanya bali wangetumia njia ya kistarabu kuweza kuwatawanyisha. Nimeshuhudia wanafunzi wakitandikwa ovyo na askari polisi huku wakitawanyika barabarani wangeweza kugongwa na magari na kusababisha matatizo mengine nimekasirishwa na kitendo hicho na wahusika wakiwemo Idara ya elimu wanapaswa kufatilia jambo hili,"alisema Nyerere.

Nyerere alisema siku zote wamekuwa wakitoa wito kwa wazazi kuacha kutoa michango isiyokuwa na tija pale wanapoombwa na wanafunzi kupitia walimu lakini wamekuwa wakiona kauli hiyo ni kama maneno ya kisiasa.

Alisema kitendo cha wanafunzi kuchangia shilingi elfu moja ili wafanyishwe mitihani ya taaluma na michezo kwa ahadi ya kupewa zawadi mbalimbali ambazo ni hewa, si cha kiungwana na kinapaswa kupigwa kwa nguvu zote.

"Tulishasema sana kuhusiana na michango ambayo haina kichwa wala miguu kuachwa lakini bado tumekuwa tukionekana maneno hayo kama ya kisiasa lakini leo wazazi wenyewe wameshuhudia wanafunzi wakichapwa viboko kwa kutafuta haki yao. Lakini katika hili lazima hatua zichukuliwe kwa wahusika na hata kama kutakuwa na mwalimu amehusika katika suala hili na ufanywe utaratibu wa kila mwanafunzi aliyechangia elfu moja yake arudishiwe maana waslitapeliwa,"aliongeza Nyerere.

Hivi karibuni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Musoma waliandamana hadi kituo cha polisi Musoma na baadaye katika makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, wakilaumu kudaiwa kuchangia fedha na kutapeliwa. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo