Kuna madai kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa katika jijini Dar es Salaam
wamekuwa wakiwatoza Sh. 2,000 watu wanaokwenda katika ofisi zao ili
kugongewa mihuri.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imewaonya baadhi ya watendaji wa mitaa jijini Dar es Salaam wanaodaiwa kuwatoza fedha wananchi kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua za sheria.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, akizungumza katika mahojiano na Radio One, alisema zoezi la vitambulisho linagharamiwa na serikali kwa asilimia 100, hivyo hairuhusiwi mtendaji yeyote kumtoza fedha mwananchi.
Alisema zoezi linaendelea katika wilaya za Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar na kuwa wanaopuuza kupata vitambulisho vya taifa watapata athari ikiwamo kushindwa kupata huduma mbalimbali kama kufungua akaunti au kupata ajira. --- via NIPASHE