Mwili
wa marehemu Dokta Sengondo Mvungi aliyefariki dunia nchini Afrika
Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu unatarajiwa kuwasili nchini leo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na na tume ya mabadiliko ya katiba na upande wa familia, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam utapelekwa moja kwa moja katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Mwili huo wa marehemu Dokta Mvungi kesho utafanyiwa misa katika kanisa la mtakatifu Joseph na baadaye kuagwa kwenye viwanja vya Karimjee, ambapo jumapili utasafirishwa kwenda wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Mazishi.
Taarifa hiyo imesema marehemu Dokta Mvungi anatarajiwa kuzikwa jumatatu novemba 18 mwaka huu Kisangara Juu wilayani Mwanga.