Maafisa
wa Marekani wameharibu zaidi ya tani 6 zilizokamatwa za pembe za tembo,
vinyago na vifaa vingine vya mapambo vinavyotokana na pembe hizo, na
kutoa ujumbe dhidi ya ujangili.
Vifaa hivyo vilikamatwa kutoka kwa wafanyabiashara haramu, wachuuzi na watalii katika vituo vya kuingilia nchini Marekani baada ya kupigwa marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani kuanzia mwaka 1989.
Shehena hiyo ya pembe za ndovu iliyokuwa karibu mita tatu za ujazo iliingizwa katika mashine ya kuvunja mawe jana Alhamis katika kituo cha huduma za wanyamapori nje kidogo ya mji wa Denver, katika jimbo la Colorado.