MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI, ABSALOM KIBANDA AANGUA KILIO UKUMBINI BAADA YA KUTANGAZWA

Mshindi  wa  tuzo ya Daudi Mwangosi Absalom Kibanda ambae ni mwenyekiti wa jukwaa la  wahariri akibembelezwa na mkewe  baada ya  kuangua kilio ukumbini mara baada ya kutangazwa mshindi  wa tuzo hiyo leo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Tido Muhando (kulia) akimkabidhi tuzu Absolom Kibanda mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi 
 
Mgeni  rasmi katika hafla  hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw  Tido Mhando  wa tatu  kulia  akimkabidhi mshindi  mfano  wa hundi ya Tsh milioni 10  Absalom Kibanda tuzo  yenye  thamani ya Tsh  milioni 10,0000 katikati ni mjane  wa Mwangosi  Itika Mwangosi  wa kwanza  kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na  rais  wake  Keneth Simbaya. =======                                                                                                                                              MHARIRI Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd. Absalom  Kibanda ameibuka mshindiwaTUZO ya uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi iliyoandaliwa na Muungano wa Klabu za waandishi wa Habari nchini (UTPC)  na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 10.

Kibanda alitangazwa leo Jijini Mwanza na Jopo la Majaji walioteuliwa kufanya mchakato wa kumtafuta mwaandishi wa Habari bora kwa mwaka huu kwenye hafla fupi katika Hoteli ya JB Belamont  na kuhudhuliwa na Wahariri wa Vyombo vya Habari, viongozi wa UTPC,Viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini , Wanahabari na Wageni mbalimbali zaidi ya 120 kutoka ndani na nje ya Tanzania' Mjumbe  wa Kamati ya Majaji hao Hamza Kassongo kwa idhini ya Mwenyekiti wake Nkwabi Mwanakilala alisema kwamba Jopo la Majaji lilitembea Mikoa mbalimbali nchini kupita na kufanya utafiti kwa waandishi wa habari na wahariri wanaotekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi na kupambana na vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji kutoka kwa viongozi wa serikali, wanasiasa na makundi mbalimbali ikiwa ni lengo la kuwatisha waandishi hao.

Kassongo aliwataja majaji wengine wanne ambao walitumia muda kufanya uchambuzi wa kumpata mshindi kuwa ni pamoja na Nkwabi Mwanakilala (Mwenyekiti), Hamza Kassongo, Leila Sheikh, Dr. Ayoub Ryoba na Rosemary Mwakitwange(wote wakiwa wajumbe wa jopo la majaji ambao wametekeleza majukumu yao baada ya kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kufuata vigezo vilivyowekwa.Msemaji wa jopo hilo la Majaji hao aliongeza kuwa mshindi wa Tuzo hiyo ambaye ametangazwa amekidhi vigezo na hakuna uchakachuaji na wakubaliane na uamuzi wa jopo hilo na kisha alimwomba Leila Sheikh kupita mbele kumtangaza mshindi wa Tuzo hiyo ambapo alimtangaza Kibanda kuwa mshindi wa waandishi wa habari nchini kwa mwaka huu baada ya kushinda vigezo kumi viliyoainishwa..
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo