KINANA AWASILI MTWARA ASUBUHI HII, YUPO NA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO NA NAPE

*NI MAANDALIZI YA KUANZA ZIARA YA SIKU 22 KATIKA MIKOA YA RUVUMA NA MBEYA

*LEO ANAKUTANA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA MSASI.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasilimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege mjini Mtwara asubuhi hii, tayari kwa safari ya kwenda katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanza ziara yake ya siku 22 katika mikoa hiyo kesho. Kabla ya kuwasili katika mikoa hiyo, akiwa mkoani Mtwara leo atakutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayya Masasi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakisalimiana na viongozi wa CCM baada ya kuwasili na Kinana mjini Mtwara asubuhi hii.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Joseph Simbakalia, Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Kinana akiwa na viongozi wa mkoa wa Mtwara.Picha na Bashir Nkoromo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo