HOT NEWS: DKT. WILBROAD SLAA ATOA KAULI NZITO KUHUSU WARAKA ULIOSAMBAA KUMHUSU ZITO KABWE

zittoManeno haya yametoka kwenye ukurasa wa facebook wa mbunge Zitto Kabwe na yamesemwa na viongozi wa Chadema kama Dr Wilbroad Slaa,Edwin Mtei na Mabere Marando kuhusu waraka uliosambaa kumhusu Zitto Kabwe.

Post ya Zitto Kabwe inaanzia hapa:-

Dr. Willbrod Slaa : ” Hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wetu kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu”

” Waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara nyeti ya serikali chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na nafasi zao”

Edwin Mtei : ” Haya mambo hayatubabaishi tunajua ni uongo uliotungwa ili kutugombanisha. Kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile. Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi lengo kutuvuruga”

Mabere Marando:  ”Andishi hili ni feki nimeliangalia andishi lote. Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema Chadema”

Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka ‘like’ kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?

Chanzo:millardayo.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo