Hatujui kama ni filamu ama maisha ya kweli, lakini muonekano mpya wa
muigizaji wa filamu, Vincent Kigosi aka Ray umewachefua wengi na wanadai
kuwa amechemka vibaya.
“Sasa c muotee kitu gani kinakuja, au nami nimegeukia Bongo Fleva,” amechokoza Ray kwenye picha alizoziweka kwenye Instagram.
Picha hizo zinamuonesha akiwa amejichora tattoo nyingi mkononi na
huku kichwani akiwa amezinyoa nywele za utosini na hivyo kuonekana kama
mtu mwenye upara wa asili.
