HATARI: MUME AUKATA MGUU WA MKEWE NA KUUTENGANISHA!!!!! TAHADHARI PICHA ZINATISHA

Hali ya wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao inayosifiwa kuwa ni Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane mwaka huu. Katika mazungumzo yake huyu binti alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa mahari na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi kurudi wala mama hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani. (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)
Samahani kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo ambao wanawake wanaupitia. juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume alipitisha panga mithili anakata muwa( Kumbuka tupo kwenye maandalizi mazito ya kuandimisha siku 16 za kupinga ukatili dhili ya Wanawake)
Mama mzazi wa binti aliyekatwa mguu na mkwe wake akilia kwa uchungu mkubwa alipokuwa anaelezea kisa kilichomkumba binti yake. Ni huzuni kubwa sana ukivaa viatu vya familia hii. Mama anasema kwa utamaduni wao baba wa mtoto aliyekatwa yaani mume wake ndiye mwenye dhamana ya kuamua mtoto arudi nyumbani au aendelee kubaki ka mume fedhuli aliyemgeuza mwenzake ni pingili la muwa.
Juu ni mama na chini ni binti akiwa na mawazo juu ya kupoteza mguu wake kwa sababu tu mume kaamua kuukata. Huyu binti ameathirika sana kisaikolojia kutokana na tatizo hilo la kukatwa mguu wake na mume wake. hivyo anaomba asaidiwe arudi nyumbani kwa wazazi wake, au popote pa kuishi ilimradi aondolewe kwenye mazingira yale aliyopatia mkasa huo. Mbaya zaidi baba mkwe wake anamwambia "wewe unaona raha kulala kitandani wakati mtoto wangu analala chini jela) kwa kauli hiyo huyu binti yupo hatarini zaidi. wanaweza kumuua wapoteze ushaidi. hata hivyo binti aligusia sababu ya kufanyiwa unyama huo ni mwanaume kuwa na mwanamke mwingine na kwamba alishahamishia mapenzi huko, na kumuona yeye kama dudu mtu. (Wakati tunaendelea na maadhalizi ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake, bado hali ni tete)
Hawa ndio Washika dau wetu wakubwa serikalini. wanasimamia Wizara ya Jinsia Maendeleo ya Jamii na Watoto. jamani waheshimiwa sana mko wapi? huku wanawake twafaaa, mnatusaidia vipi? viti vya bunge vinakalika vipi kwa hali hii? ni lini wanawake tutapaza sauti zetu ili dunia ijue unyama huu unaoendelea dhidi ya wanawake wa Tanzania? Wanawake Hatuna AMANI kabisa ndani ya nchi yetu. Wizara na Taasis mbalimbali, Wadau wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, kuna jinsi ya kumsaidia huyu mama kwa kumuondoa pale kwenye ile nyumba na akapewa makao salama? Usikose kufuatilia Joyce Kiria Wanawakelive EATV na hapa kwenye ukurasa wetu, ili upate mkasa huu wakati tunajipanga kuendelea na mapambano ya Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake.
 
PICHA KWA HISANI YA WANAWAKELIVETV.COM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo