Na Yohane Gervas, Rombo
POLISI wilayani Rombo inamshikilia mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la Martini Shayo (71) mkazi wa Kijiji cha Mengeni
Chini Wilaya ya Rombo kwa kosa la kumbaka mwanaye wa kike mwenye umri
wa miaka sita.
Mkuu wa Polisi (OCD) wa Wilaya ya Rombo, Ralph Meela akizungumza na
mtandao huu alisema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 18, 2013 majira ya
saa saba mchana katika Kijiji cha Mengeni Chini Tarafa ya Mengwe
wilayani hapa.
Aidha aLISEMA mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye jina lake
limehifadhiwa alipata maumivu makali sehemu zake za siri hivyo baada ya
polisi kupata taarifa hizo walimwandikia PF3 na kwenda kupatiwa matibabu
katika hospitali ya Huruma.
Mke wa mtuhumiwa, Anna Shayo ambaye pia ni mama wa mtoto aliyebakwa
amesema kuwa mume wake alimwita mwanae amfuate ndani lakini baada ya
muda mfupi alimsikia akiwa anapiga kelele na alipomfuata ndani alimkuta
baba akiwa anamfanyia mwanae kitendo hicho.
Aidha ameongeza kuwa baada ya hapo alipiga ukunga kuomba msaada na
kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo polisi walifika na kumkata
mtuhumiwa mara moja na kumuweka chini yaulinzi.
Kwa mujibu wa mtoto
aliyebakwa amesema kuwa baba yake alikua na mazoea ya kumchezea wakati
mama yake hayupo na kisha alikua akimpa pipi ili asiseme kwa mama yake.
Tukio hilo limeibua hisia tofauti tofauti kwa wakazi wa Rombo huku
wengine wakilihusisha na imani za kishirikina na kuomba vyombo vya dola
kulifanyia uchunguzi wa kutosha ili kudhibiti kabisa matukio hayo.
CHANZO:thehabari.com