Mtoto mmoja aliyefahamika kwa Jina la Malaika Jackson amefariki
dunia Muda huu ( saa kumi jioni ) baada ya kuangukiwa na Jiwe
kubwa lililoporomoka wakati baba yake akichimba kokoto katika
mlima Giza, maarufu kama mlima wa Rada uliopo maeneo ya Kiseke,
Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza
Kabla
ya kufikwa na mauti hayo, Mtoto huyu alikuwa na baba yake
mzazi aliyefahamika kwa jina la Jackson Ismail, mama yake mzazi
na mdogo wake wakipata chakula cha mchana baada ya kuponda
mawe kutwa nzima.....
Wangali
wakipata chakula hicho, baba aliwahi kumaliza na hivyo
kuendelea na kazi hiyo ya kuponda mawe huku mkewe na watoto
wakimalizia kupata chakula....
Wakati
bwana Ismail akiendelea kuyaporomosha mawe hayo,ghafla alisikia
mtikisiko mkubwa na hivyo kumtaka mkewe na watoto watoke
haraka.....
Mama akiwa na mtoto mchanga waliwahi kunyanyuka na kutoka,lakini kabla binti Malaika mwenye umri wa miaka mitano hajatoka, jiwe kubwa lilimuwahi na kumkandamiza na kumfanya afariki dunia papo hapo....