POLISI MKOANI NJOMBE WAKAA NA BODABODA KUJADILI HALI YA KUTISHA ILIYOIBUKA DHIDI YAO


Siku Kadhaa zilizopita Madereva wa Bodaboda waliingiwa na hali ya wasiwasi kutokana na matukio kadhaa yaliyotokea Mkoani Njombe dhidi yao na hivyo kuhatarisha usalama wa kazi zao.
 
Madereva hao wameonekana kuingiwa na hofu hiyo Ikiwa ni Wiki Moja tu Kupita Tangu Dereva Mwenzao wa Bodaboda Wa kituo cha Eneo la Sangamela Mjini Njombe Kutekwa na kuuawa Kinyama na Watu Wanaosadikika Kuwa ni Majambazi Ambapo Mtu mmoja Aliyekodi Pikipiki Kwa Kijana Huyo Ndiye Anasadikika Kusababisha Mauaji ya Dereva Huyo.

Sanjari na Hilo Lakini Pia Hivi Karibuni Kijana Mmoja Ambaye Hakujulikana alikutwa ametekwa na kutupwa Kwenye Maeneo ya Kata ya Njombe Mjini Ambaye Inasadikika Kuwa naye Alikuwa Dereva wa bodaboda.

Kutokana na matukio Hayo Madereva wa Bodaboda Mjini Njombe Wameingiwa na Hofu na Kuanza Kufikiria Mbinu Mbalimbali za Kuweza Kujilinda Bila Kupata Majibu ya Haraka.

Hivyo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani Limelazimika Kuwaita na Kujadili Namna ya Kuimarisha Ulinzi Katika Biashara zao.

Picha na Michael Ngilangwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo