PICHA ZA UTUPU ZA WATU MAARUFU ZAANIKWA MITANDAONI...FBI WAANZA UPELELEZI



Idara ya upelelezi ya nchini marekani FBI imetoa tamko kuwa  inachunguza kwa ukaribu madai ya maelfu ya accounts za watu maarufu kutekwa,na kinachotafutwa hasa ni picha za utupu za watu hao maarufu ambazo zimekua zikianikwa mitandaoni bila ya muwekaji kujulikana.

Katika tamko la FBI liliripotiwa na NBC News, wameeleza kuwa walikuwa wanafahamu kuhusu vitendo vya wezi wa njia za mtandao kuhack mafaili ya watu maarufu waliyoyatunza kwenye simu zao kwa application za kutunza mafaili mtandaoni na kwamba wameanza kufanya uchunguzi.
  
"The FBI is aware of the allegations concerning computer intrusions and the unlawful release of material involving high profile individuals and is addressing the matter.” Inaeleza sehemu ya tamko hilo.
 
Sakata  hili limemkumba mshindi wa tuzo ya Oscar Jennifer Lawrence ambaye picha zake  za uchi ziliachiliwa mtandaoni  pamoja  na  Kate Upton na Mary Elizabeth Winstead.

Nae msemaji wa Apple anaehusika na applications za kutunza mafaili online ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza pia kufanya upelelezi juu ya tukio hilo ili kubaini kama uvujaji wa picha hizo umesababishwa na iCloud . 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo