AAMUA KUJINYONGA KUKWEPA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MKOANI IRINGA, KISA HOFU YA KUFELI

 
 
Askari  kanzu  akikagua  mwili wa mwanafunzi  huyo  leo
  barua yenye ujumbe aliouacha marehemu huyo.
--------
Mwanafunzi  aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hiyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  huu  kuwa  tukio  hilo limetokea muda wa  kati ya saa 12 na saa 1  usiku wa jana baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea 'kurisiti'  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kwani  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.

Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi naye kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha.
Kuona habari hii na picha nyingi za tukio hilo tafadhali bonyeza link hiyo hapo mbele ya chanzo cha habari hii www.matukiodaima.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo