MAKAMU WA RAIS DK BILAL AKIRI KUWEPO KWA UHABA WA WAALIMU NA WATAALAM WA SAYANSI NCHINI

Serikali imekiri kuwa bado kuna uhaba mkubwa wa walimu na wataalam wa masuala ya sayansi nchini na kuongeza kuwa kuna haja ya kubuni mbinu mpya zitakazojenga mazingira ya kuwavutia wanafunzi kusoma masomo hayo na walimu wa masomo hayo kuwa na moyo zaidi wa kufundisha.

Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilali ameyasema hayo muda mfupi baada ya kufungua rasmi jengo la kituo cha walimu lililopo chuo kikuu kishiriki cha Elimu DUCE kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam, jengo lililojengwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa sayansi, teknolojia na elimu ya juu uliotekelezwa na benki ya dunia kwa kipindi cha miaka mitano na kushirikisha taasisi za elimu ya juu kumi na tano.

Makamu wa rais amesema pamoja na hitaji kubwa la walimu wa sekondari na vyuo vya elimu ya juu, hadi sasa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia ishirini ya walimu wanaofundisha sekondari nchini ndio wenye degree huku uhaba wa walimu wa sayansi ktika shule hizo ukiwa ni 25,000.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo