DIWANI ATOA RAI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE WILAYANI MAKETE KUJIANDAA NA MTIHANI WA TAIFA

Wanafunzi shule za sekondari wilayani Makete wameaswa kuwa makini ktk maandalizi yao ya kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu

Hayo yamesemwa na Mh.diwani wa kata ya Ukwama wilayani hapa Smith Sanga akiwa ktk mahafali ya kwanza tokea kuanza kwa shule ya sekondari ya kata ya Ukwama iliyoanza rasmi mwaka 2010

Diwani huyo amesema kuwa wanafunzi wa shule hiyo wengi wao wamekuwa wakikabiliwa na janga la upataji mamba ovyo zinazosababishwa na wanafunzi hao kuishi mtaani ambapo mazingira hayo ni hatari sana kwa mtoto wa kike

Jumla ya watahiniwa 35 wa kidato ha nne ndio wanaotegemewa kufanya mtihani wa kidato cha nne ktk shule hiyo ya kata iliyoanza kujengwa mwaka 2005na kuanza kupokea wanafunzi Rasmi mwaka 2010 hivyo ktk hali hiyo wanafunzi hao ndio waliozindua kuanza mafunzo yao hapo mwaka 2010 na mwaka huu ndio wamemaliza kwa mara ya kwanza ktk shule hiyo

Akizungumza nasi Mwl.Matokeo John amesema wazazi wengi wa watoto hao wamekuwa wakiwatorosha wanafunzi na kuwapeleka mijini kufanya kazi mbalimbali hivyo kupungua kwa idadi kubwa ya wanafunzi shuleni hapo

Pia Mh.Diwani amezitaja baadhi ya changamoto ambazo wanafunzi wamezisoma ktk risala yao kwa mgeni Rasmi Afisa elimu Wilaya Bw.Jacob Meena ambapo amesema ukosefu wa bweni za kulala wanafunzi ambapo kuishi mitaani kwa wanafunzi kunaongeza wimbi la upataji mimba kwa watoto wa kike, na upungufu wa walimu hasa upande wa masomo ya sayansi

Na:Furahisha Furahisha Nundu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo