Ben Komba, Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani BIBI.MWANTUMU MAHIZA ametoa msaada wa mabati 100 kwa mwandishi wa habari mkongwe Mkoani Pwani BW.AMIR LUGUNGULO ikiwa kama msaada wa kiutu ili kumwezesha mwandishi huyo kumalizia nyumba yake.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo wa mabati, Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI.MWANTUM MAHIZA amesema amefikia hatua hiyo baada ya mwandishi huyo mkongwe kumuomba msaada huo adhimu ili aweze kukamilisha nyumba yake iliyopo maeneo ya Tabata.
BIBI.MAHIZA ameongeza kwa kuwataka waandishi wasisite kuomba msaada wnapokuwa wana matatizo ambayo yanawakabili, kwani hiyo ndiyo hali ya kilimwengu, badala ya kutumia mbinu za udanganyifu na utapeli ili kujipatia fedha, mbali ya kukabidhi bati 100 kwa mwandishi huyo mkongwe pia alimkabidhi shilingi laki 1 kwa ajili ya kubebea bati hizo.
Akipokea msaada huo Mwandishi AMRI LUGUNGULO amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Pwani kwa msaada huo na amemuombea maisha marefu na mafanikio katika kazi zake, kwani msaada huo ni mkubwa kulinganisha na kipato anachopata katika mazingira ya kazi yake.
Aidha BW.LUGUNGULO amewaasa waandishi wenzie kutosita kuomba msaada wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali, badala ya kutumia mbinu za kiujanjaunja ili kujipatia kipato.