RAY C ASEMA HAJAOKOKA WALA HANA VIRUSI VYA UKIMWI



Mwanadada  anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni tena  akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.


Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.


Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.


“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.

 
“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo