Kamati
ya uongozi na kamati ya kanuni ya bunge zimelazimika kukutana kwa
dharura bungeni mjini Dodoma baada ya baadhi ya wabunge kuomba muongozo
wa spika kusitisha shughuli nyingine za bunge ili kulijadili suala la
mgogoro wa wafanyakazi wa Tazara kwa madai kuwa mgogoro huo unaathiri
uchumi wa nchi na jamii kwa ujumla.
Naibu
spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai ndiye
aliyeamuru kamati hizo kukutana kwa ajili ya kulijadili suala hilo na
kulitoloea maamuzi baada ya mh suzan kiwanga mbunge wa chadema kusimama
kwa mujibu wa kanuni ya bunge ya 47 na 48 kulitaka bunge kusitisha
shughuli nyinginezo na kulijadili suala la mgogoro wa wafanyakazi wa
Tazara.
Waziri
wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,uratibu na bunge Mh William Lukuvi
akasimama ambapo licha ya kukiri kuwepo kwa tatizo hilo amedai kuwa
mejimenti na bodi ya Tazara inahusisha nchi mbili za Tanzania na zambia
na kwamba serikali ya tanzania haiwezi kutoa maamuzi bila ya kuihusisha
serikali ya zambia na kwamba suala hilo linaendelea kushughulikiwa
Majibu
hayo ya Mh lukuvi yakamlazimisha mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani
bungeni Mh Tundu Lisu kusimama na kumtaka naibu spika kutoa uamuzi juu
ya suala hilo kwa kuwa bunge si serikali
CHANZO:ITV