WAZIRI MKUU PINDA KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO LONDON JUMANNE AGOSTI 6, 2013

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda hapo Ubalozini siku ya Jumanne (tarehe 6 Agosti 2013) kuanzia saa Kumi na Nusu alasiri (1630 hours au 04.30 p.m.).
 
Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi na ushirikishwaji wa Diaspora. Aidha atajibu maswali kutoka kwa wananchi hao.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMAPILI (4 AGOSTI 2013)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo