RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON AKARIBISHWA ZANZIBAR NA RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMED SHEIN

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,(katikati) aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake. Kushoto ni Chelsea Clinton,ni Mtoto wa Rais Mstaafu huyo wa Marekani
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na  Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya mazungumzo yao
 Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chelsea Clinton,akipiga mpira kama ishara ya kufungua mpambano wa Timu za wachezaji wa zamani katika sherehe za Ziara ya Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,kukagua miradi mbali mbali katika nchi za Afrika iliyo chini ya ufadhili wa Taasisi yake ya CLINTON FOUNDATION katika uwanja wa Amaan leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Marekani  Chelsea Clinton,baada ya kufungua mpambano wa Mpira wa Miguu kwa timu za Wachezaji wa Zamani uliofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium,(katikati) Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,wakipata maelezo kutoka kwa  Bruno Mnnen,wakati walipotembelea katika banda la utoaji wa huduma ya uchunguzi wa Damu ya Maleria pamoja na Vyandarua,(Clinton Health Access Initiative-CHAI) katika ziara yake Clinton kuangalia miradi mbali mbali katika Nchi za Afrika,(wapili kushoto) Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chelsea Clinton
Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo