WAFANYABIASHARA SOKO LA MAJENGO DODOMA KUGOMA KULIPA USHURU

Wafanyabiashara zaidi ya 2000 wa soko kuu la Majengo Manispaa ya Dodoma wametishia kutolipa ushuru kuanzia Septemba mosi mwaka huu kwa madai kuwa Manispaa ya Dodoma imeshindwa kutatua kero za muda mrefu zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa vyoo na kushindwa kudhibiti wafanyabiashara holela katika maeneo yasiyo rasmi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara hao Godson Rugazama ambaye anasema licha ya kupeleka madai yao mara kwa mara kwa uongozi wa Manispaa ya Dodoma bado hayafanyiwi kazi

SOURCE:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo